Waziri Dkt. Gwajima na UWT kuedeleza kumkomboa mwanamke kiuchumi

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wamejadili kuimarisha ushirikiano kwenye ajenda za kuendelea kumkomboa Mwanamke Kiuchumi, kiongozi, kijamii na kupambana na ukatili wa kijinsia.

Akizungumza na Katibu Mkuu wa UWT Ndugu Jokate Mwegelo Ofisi za Makao Makuu Jijini Dodoma 21 Novemba, 2023 Dkt. Gwajima amesema wameweza kujadiliana juu ya mipango mbalimbali ya kisekta inayohusu kumkomboa mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwa ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na kuendelea kuhakikisha Wanawake wanainuliwa kiuchumi ikiwa ni dhamira thabiti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kujenga na kuimarisha jamii iliyo bora na rafiki kwa Watoto na Wanawake wote nchini.

Chapisha Maoni

0 Maoni