Mwanariadha mlemavu Pistorius kuachiwa huru Januari 2024

 

Mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius anatarajia kuachiwa huru kwa msamaha wa Bodi ya Parole, baada ya kukaa jela miaka 11 akitumikia kifungo kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Pistorius alimpiga risasi kadhaa mpenzi wake huyo aliyekuwa bafuni katika Siku ya Wapendanao mwaka 2013, na baadae kudai kuwa alidhania kuwa ni kibaka aliyeingia nyumbani kwao huko Pretoria, Afrika Kusini.

Pistorius, sasa anamiaka 37, na alihukumiwa na Mahakama ya Afrika Kusini mwaka 2016, kutumiakia kifungo cha miaka 13 jela na miezi mitano, baada ya kumtia hatiani kwa mauaji ya mpenzi wake huyo.

Bodi ya Parole ya Afrika Kusini imepanga kumuachia huru Oscar Pistorius Januari 5, mwaka 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni