Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini
Uingereza itafanya kambi maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia
kwa wagonjwa wenye changamoto za maradhi ya nyonga na magoti kuanzia tarehe 27.11.2023
hadi 01.12.2023.
Akielezea kambi hiyo,
Daktari Bingwa wa Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti, Dkt. Shilekirwa Makira
amesema wagonjwa watakaonufaika na huduma hizo ni pamoja na wenye matatizo ya
nyonga zilizosagika zenye maumivu makali na magoti yaliyosagika.
Dkt. Makira ameongeza kuwa
watu wenye changamoto hizo watabadilishiwa kwa kuwekewa nyonga na magoti bandia
kitu kitakachowafanya waondokane na maumivu wanayoyapata kabla ya nyonga zao
kubadilishwa.
“Tungependa watu wajitokeze
na kujisajili mapema kabla ya tarehe 27.11.2023 ili hospitali iweze kufanya
maandalizi stahiki ikiwemo pamoja na kufanya vipimo vya awali ambayo ni muhimu
kabla ya kufanya upasuaji huu” amesisitiza Dkt. Makira
Dkt. Makira amefafanua kuwa
kwa wale waliojiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya, mfuko unagharimia zaidi
ya asilimia 90, pia bima zingine zinagharimia matibabu haya hivyo wasisite
kujitokeza kuchangamkia fursa hii adhimu.
Kwa maelezo zaidi, ushauri
au kuweka miyadi (appointment) unashauriwa kuwasiliana na Madaktari Bingwa
Idara ya Magonjwa ya Mifupa na ajali ambao ni Dkt. Makira simu namba
0765958302, Dkt. Abuu 0715219175 na Dkt. Amos 0683680522.
0 Maoni