Basi laigonga treni na kuua watu 13 Manyoni

 

Watu 13 wamefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ally's Star kuigonga treni ya mizigo huko Manyoni mkoani Singida.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manyoni Dk. Furaha Mwakafilwa amenukuliwa akisema kwamba wamepokea miili ya watu 13 pamoja na majeruhi 32.

Basi hilo la Kampuni ya Ally's lenye namba za usajili T 178 DVB lililigonga treni ya mizigo leo alfajiri majira ya saa 11, katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya Manyoni.

Chapisha Maoni

0 Maoni