Paa la kanisa laangukia waumini na kuua watu tisa

 

Watu tisa wameripotiwa kufa na wengine 20 kunasa, baada ya paa la kanisa kuangukia waumini nchini Mexico.

Vyombo vya nchini humo vimesema watu 49 wamepelekwa hospitali, baada ya paa la kanisa hilo la Santa Cruz lililopo mji wa Ciudad Madero kuanguka.

Polisi wa jimbo la pwani la Tamaulipas wamesema kwamba waumini wapatao 100 walikuwa kwenye ibada hiyo ya ubatizo wakati paa hilo lilipoanguka.

Idadi kubwa ya watoto inaaminika kuwa miongoni mwa walionasa chini ya paa, jitihada za kuwakwamua zinaendelea.

Chapisha Maoni

0 Maoni