Ngorongoro yashinda tuzo ya Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika

 

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro limetangazwa kuwa mshindi katika kipengele cha kivutio bora cha utalii barani Afrika (African leading tourist Attractions) na kupewa tuzo na mtandao wa World travel awards.

Tuzo hiyo imetolewa usiku huu wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika hotel ya Atlantis The Royal Dubai   katika nchi za Falme za Kiarabu ambapo Ngorongoro imeshinda tuzo hiyo baada ya kushinda vivutio vingine vya utalii barani Afrika ambavyo ni tableMountain, Hartbeespoort aerial cableway, V& A Waterfront, Ruben Island vya Afrika Kusini, Ziwa Malawi, Okavango Delta ya Botswana, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Pyramis of Giza ya Misri.

Tuzo hiyo imepokelewa na Meneja wa Huduma za Utalii NCAA Bw. Peter Makutian kwa niaba ya uongozi wa shirika.

Chapisha Maoni

0 Maoni