Mtu mwenye silaha auwa watu 16 Lewiston, Marekani

 

Watu wapatao 16 wanahofiwa kufa katika tukio la kushambuliwa kwa risasi kwenye mji wa Lewiston, Maine nchini Marekani.

Polisi wa mji huo wamemtaja mtuhumiwa wa mashambulizi hayo kuwa ni Robert Card mwenye umri wa miaka 40, na kusema kuwa anasilaha na ni mtu hatari.

Mji huo mdogo wa Lewiston, Maine umefungwa, wafanyabiashara wameambiwa wafunge biashara zao na watu wameagizwa kukaa nyumbani.

Mamia ya maafisa wa polisi wapo katika msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo aliyefanya mauaji hayo kwenye hoteli na eneo la michezo wa shabaha ya kulenga chupa.

Chapisha Maoni

0 Maoni