Israel yasema itakuwa ngumu kushuhudia kinachotokea Gaza

 

Watu waliokufa kwa shambulizi lililofanya na kundi la Hamas nchini Israel wamefikia 1,200, huku pia watu 900 wakiuawa huko Gaza katika mashambulizi ya Israel ya kulipa kisasi.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel amesema picha zinazotoka Gaza zitakuwa ni vigumu kwa mtu kushuhudia.

Wakati huo huo ndege ya kwanza ya Marekani iliyobeba silaha imewasili kusini mwa Israel kupeleka msaada wa silaha.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amempigia simu Rais wa Marekani Joe Biden na kumshukuru kwa kuiunga mkono Israel.

Chapisha Maoni

0 Maoni