Mkuu wa wilaya ya Kwimba Ngw'ilabuzu Ludigija ameiagiza
wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kutatua changamoto ya
ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa kata za Shilembo na Ilula kwa
kuvuta maji kutoka maeneo jirani au kuchimba visima ili wakazi hao wapate maji.
Akiwa katika mwendelezo wa kusikiliza na kutatua kero za
wakazi hao Ludigija amesema maji ni muhimu hivyo RUWASA wanatakiwa kufanya
jitihada za kuhakikisha maji yanafika kwa wakazi wa kata hizo.
"Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anaendelea
kuleta fedha za miradi ya maji ili kumtua mama ndoo kichwani sasa niwatake
RUWASA muangalie uwezekano wa kufikisha maji hapa," amesema Ludigija.
Akizungumza mwa niaba ya wakazi wa kata hizo Mwalu Joseph
amesema wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji na kushindwa kufanya
shughuli zingine za maendelo.
"Tunateseka sana kupata maji tunatembea zaidi ya
kilometa tisa kwenda kutafuta maji tunamuomba Rais atusaidie tupate japo visima
au amji ya Ziwa Victoria ili tuepukane na adha hii," amesema Mwalu.
0 Maoni