Brian Njagi wakili feki wa Kenya aliyeshinda kesi zote 26

 

Hali ya taharuki imeibuka baada ya Chama cha Wanasheria Kenya kubaini kuwa mwanaume mmoja anayefanya shughuli ya uwakili si wakili na wala hana leseni ya kuwa wakili wa Mahakama Kuu.

Wakili huyo kanjanja Brian Mwenda Njagi amesimamia kesi 26 katika Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Rufaa na kushinda kesi zote hizo.

Njagi anayedai kuwa ni wakili wa Nairobi, alikamatwa jana na mamlaka za nchi hiyo kwa kujifanya kuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Kikosi maalum Chama cha Wanasheria Kenya tawi la Nairobi RAT, kilimkamata Njagi baada ya kupata malalamiko ya watu kuwa ni laghai.

Baada ya kusamba taarifa za kukamatwa kwake, baadhi ya Wakenya kupitia mitandao ya jamii wamekuwa wakimpongeza wakili huyo kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kisheria kuliko waliosomea.

Chapisha Maoni

0 Maoni