Serikali yagawa magunia 1,058 ya mahindi kwa waliohamia Msomera

Serikali ya awamu ya sita imeendelea kutimiza ahadi ya kugawa chakula (mahindi) bure kwa wananchi waliohama kwa hiari kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Mkoani Tanga

Dhumuni la kugawa mahindi hayo kwa wananchi kila baada ya miezi mitatu (03) ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali kutoa chakula bure kwa wananchi hao kwa muda wa miezi 18 wakati wakiendelea kuzoea mazingira mapya waliyohamia kabla ya kulima na kuvuna kupitia mashamba waliyopewa na Serikali.

Katika mgao wa mwezi oktoba jumla ya gunia 1,058 zenye tani 95.22 zimegawanywa kwa kaya 529 ambapo baada ya mgao huo Wananchi hao wameendeela kuishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali katika huduma ya chakula na kuendelea kuboresha huduma za kijamii.

Chapisha Maoni

0 Maoni