Mwalimu auawa shuleni kwa kuchomwa kisu Ufaransa

 

Mwalimu mmoja ameuawa na watu wengine wawili kujeruhiwa vibaya, katika tukio la shambulizi la kutumia kisu kwenye shule nchini Ufaransa.

Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin amesema shambulizi hilo limetokea kwenye shule ya Gambetta katika mji wa kaskazini wa Arras majira ya saa tano asubuhi.

Mtu aliyefanya shambulizi hilo amekamatwa na anashikiliwa. Kwa mujibu wa mashuhuda alikuwa akisema "Allahu Akbar", (Mungu Mkubwa) wakati akiwashambulia watu.

Mtu aliyeuawa ametambulika kuwa ni mwalimu wa lugha ya Kifaransa, na wawili waliojeruhiwa ni mwalimu mmoja pamoja na mlinzi wa shule.

Chapisha Maoni

0 Maoni