Wanamgambo wa Kiislamu wawaua raia 49 kwenye boti Mali

 

Wanamgambo wa Kiislamu wameshambulia boti kwenye mto kaskazini mashariki mwa Mali, na kuua raia wapatao 49, Serikali ya mpito ya nchi hiyo imesema.

Pia, imeripotiwa kikundi hicho kimeshambulia kambi ya jeshi, na kuwaua wanajeshi 15, huku pia wapiganaji hao wapatao 50 wakiuawa.

Kufuatia mauaji hayo Serikali ya mpito ya Mali, imetangaza siku tatu za maombolezo.

Chapisha Maoni

0 Maoni