Serikali imewatahadharisha wananchi kuacha kujenga na
kufanya shughuli za kijamii kwenye maeneo ya mabondeni, ili kuepukana na athari
za mafuriko zinazoweza kutokea na kusababisha madhara, pindi zinyeshapo mvua
kubwa kama za El Nino.
Tahadhari hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati
akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma leo Septemba 05,2023.
" Nikweli panapokuwa na mvua kubwa kama za El Nino mara
nyingi hutokea madhara ambayo yanaharibu makazi na kugharimu maisha ya watu,
hivyo Serikali katika kipindi hiki tunawapa elimu wasijenge kwenye maeneo
ambayo yanakaa maji na kama wanampango huo basi waondoke ili mvua
zitakaponyesha wasipate madhara," alisema Mhe. Khamis.
Hivi karibuni Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
ilitangaza kuanza kwa mvua za El Nino Oktoba hadi Desemba 2023 na
kutahadharisha kuweza kusababisha madhara kwa binadamu na mazingira ikiwemo
mafuriko.
0 Maoni