Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko
amekutana na Timu ya Serikali ya Majadiliano kuhusu mradi wa kuchakata na
kusindika Gesi Asilia (GNT) ili kufahamu hatua zilizofikiwa kuhusu majadiliano
hayo.
Dkt. Biteko amekutana na timu hiyo tarehe 9 Septemba, 2023
katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine
ameipongeza timu hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi hatua iliyofikiwa mpaka
sasa.
Katika kikao hicho Dkt. Biteko ameielekeza GNT kukutana na
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikiali, Inaoshughulika na mikataba ili
kuwaeleza kwa kina maendeleo na hatua iliyofikiwa hadi sasa.
Dkt. Ameitaka Timu kuwa huru katika kupokea mawazo kila
mmoja katika kujenda uelewa wa pamoja wanapofanya kukubaliana mambo.
Ametaka timu hiyo kuongeza kasi ili kukamilisha majadiliano
hayo ili mradi huo uanze kutekelezwa kwa kuwa wananchi wanausubiri kwa hamu
kubwa kutokana na umuhimu wake kwao na Taifa kwa jumla.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati,
Mhe. Judith Kapinga, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, Musa Makame na
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Petrol Lyatuu na viongozi wengine
kutoka Wizara ya Nishati.
0 Maoni