Rais Dk. Mwinyi awasili Cuba kushiriki mkutano wa G77+China

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake amewasili leo Havana, Cuba kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa kundi la 77 na China (G77+China)

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa kesho tarehe 15 Septemba ambapo Rais Dk. Mwinyi atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Katika uwanja wa ndege wa Jose Marti Rais Dk. Mwinyi alipokelewa na Balozi wa Tanzania Mhe.  Humphrey Polepole na maafisa wengine wa ubalozi wa Tanzania Havana, Cuba.

Baadae leo Rais Dk. Mwinyi atafungua rasmi ubalozi wa Tanzania nchini Cuba.

Chapisha Maoni

0 Maoni