Marekani yaonesha nia ya kushirikiana na TBN kutoa mafunzo

 

Chama cha Tanzania Bloggers Network (TBN) leo kimekutana na Afisa wa masuala ya Umma Bi Jeanne Clark pamoja na Bi. Kalisha Holmes, Afisa Habari na Mawasiliano wa Ubalozi wa Marekani katika kikao kisicho rasmi kilichoambatana na chakula cha mchana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, wanachama waandamizi wa TBN waliohudhuria walieleza mipango inayoendelea ya kukiendeleza chama chao ili kukuza kazi nzuri inayotekelezwa na chama hicho kilichozinduliwa mwanzoni mwa mwaka 2015.

Maafisa hao wa ubalozi wamesema wanavutiwa na kazi zinazofanywa na wanahabari mitandaoni na wameelezea nia ya kishirikiana na TBN katika mafunzo ili kukuza taaluma kwa kuzingatia weledi na miiko ya uanahabari.

Chapisha Maoni

0 Maoni