Novatus Dismas kuwa Mtanzania wa pili kucheza UEFA

 

Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi, anaenda kuwa mchezaji wa pili kutoka Tanzania kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), baada ya Mbwana Samatta.

Novatus mwenye umri wa miaka 21 amepata nafasi hiyo baada ya kujiunga na klabu ya Shakhtar Donesk ya Ukraine akitokea klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji.

Kwa hiyo kiungo huyo wa Stars, atacheza UEFA Champions League akiwa na timu yake mpya ambayo ipo kundi H pamoja na timu za Barcelona, Porto na Royal Antwer.

Chapisha Maoni

0 Maoni