Moto waua watu 100 kwenye harusi Irak na kujeruhi 150

 

Watu wapatao 100 wamekufa na wengine 150 wamejeruhiwa, baada ya moto kutokea kwenye harusi kaskazini mwa nchi ya Irak, chombo cha habari cha umma kimeripoti.

Haijafahamika mara moja chanzo cha moto huo, lakini taarifa za awali zinasema moto huo umetokea baada ya kufyatuliwa fataki.

Picha katika mitandao ya jamii zinaonyesha mabaki ya ukumbi uliofanyika harusi hiyo kwenye mji wa  Al-Hamdaniya katika mkoa wa Nineveh.

Vifaa vilivyotumika kujengea ukumbi huo vyenye uwezo wa kuwaka moto vimeelezwa kwamba vilichangia kuuchochea moto huo, maafisa wa Irak wamesema.

Haijajulikana bado iwapo maharusi na wapambe wao kuwa ni miongoni mwa watu waliokufa ama kujeruhiwa katika tukio hilo la ajali ya moto.



Chapisha Maoni

0 Maoni