Mfungwa Mpalestina alala na wanajeshi wanawake wa Israeli

 

Wanajeshi wanawake wa Israeli watazuia kufanyakazi kama walinzi wa magereza yenye kuhitaji ulinzi mkali, baada ya kuibuka kwa tuhuma za kufanya ngono na mfungwa Mpalestina.

Vyombo vya habari vya Israeli vimesema mwanajeshi huyo amekiri kufanya ngono na mfungwa mwanaume Mpalestina, ambaye alifanya shambulizi kubwa kwa raia wa Israeli.

Mwanamke huyo inaaminika alikuwa katika mafunzo ya kijeshi, ambayo ni lazima kupitia kwa raia wengi wa Israeli.

Kwa mujibu wa sheria za Israeli mwanamke anapaswa kulitumikia jeshi kwa muda wa japo miaka miwili na kwa wanaume muda wa miezi 32.

Jina la mwanajeshi huyo mwanamke na mfungwa wa kiume Mpalestina anayetumikia adhabu ya kifungo cha maisha hayajatolewa.

Vyombo vya habari Israeli vimeripoti pia, katika mahojiano mwanajeshi huyo ambaye amekamatwa, alidai wanawake wengine wanne nao walikuwa na mahusiano ya mapenzi na mfungwa huyo mwanaume.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni