Matukio mbalimbali katika ziara ya Rais Samia Ruangwa Lindi

 

Wananchi wakiwa na bango lenye jumbe mbalimbali wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika jambo la Ruangwa leo akiwa na mbunge wa jimbo hilo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akiangalia Akina mama (wa Kabila la Wamwera) wakiwa wamelala chini kama ishara ya heshima kubwa ya Mapokezi kwa Mhe. Rais Samia mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kilimahewa Ruangwa Mkoani Lindi tarehe 18 Septemba, 2023.

Akina Mama wa Kabila la Wamwera wakiwa wamelala chini kama ishara ya Heshima kubwa ya mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Kilimahewa Ruangwa Mkoani Lindi tarehe 18 Septemba, 2023.

Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Lindi Mhe. Teckla Ungele akicheza pamoja na Akina Mama wa Kabila wa Wamwera wakati wa shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ruangwa Mkoani Lindi tarehe 18 Septemba, 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni