MAPIGANO SUDAN: Majengo marefu yaungua moto

 

Majengo marefu yanaungua moto katika Jiji la Sudan, baada ya mapigano makali baina ya vikosi vya majeshi vinavyokinzani nchini humo.

Video iliyopostiwa kwenye mitandao inaonyesha jengo refu la kampuni ya mafuta ya Greater Nile Petroleum Oil likiwa linawaka moto.

Mashambulizi ya anga na yaaridhini yamekuwa yakiendelea Jijini Khartoum pamoja na kwenye miji mingine tangu mapigano hayo yaanze mwezi Aprili, 2023.

Mapigano hayo ya baina ya vikosi viwili vya jeshi la nchi hiyo vilivyohitilafiana yamepelekea watu zaidi ya milioni moja kukimbia nchi hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni