Kiongozi wa uvamizi jengo la US Capital 2021 jela miaka 17

 

Kiongozi wa kundi la mrengo mkali wa kulia la Proud Boys amehukumiwa kifungo cha miaka 17 jela, kikiwa ni moja ya kifungo cha muda mrefu kwa kuhusika na uvamizi katika jengo la US Capitol 2021.

Mwanajeshi huyo veteran wa Marekani Joe Biggs, 38, alihusika katika kuchochea tukio la kuvamia kikoa cha Baraza la Congress wJanuaria 6, 2021.

Biggs ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa kujitegemea wa tovuti ya habari feki ya Infowars ametiwa hatiani kwa makossa ya uchochezi na kula njama, pamoja na mashtaka mengine mwezi Mei.

Mwanachama mwingine wa kundi la Proud Boys, Zachary Rehl, alihukumia kwenda jela miaka 15, siku ya Alhamisi kwa makosa ya uchochezi na kula njama.

Januari 6, 2021 kundi la Proud Boys liliongoza tukio la kuvamiwa kwa jengo la Capitol katika jitihada za kushinikiza Baraza la Congress lisiidhinishe ushindi wa Rais Joe Biden.

Chapisha Maoni

0 Maoni