Moto ulioua watu 74 Jijini Johannesburg watoa funzo SA

 


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amesema moto ulioleta maafa katika Jiji la Johannesburg umetoa funzo kwa taifa hilo.

Watu 74 wamekufa wakiwamo watoto 12, baada ya moto huo kuunguza jengo la ghorofa walimokuwa wanaishi watu wasionamakazi, wengi wao wakiwa wahamiaji.

Watu wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika tukio hilo la ajali ya moto mbaya iliyozishtua mamlaka za Jiji.

Mapema jana, mamlaka ya Jiji la Johannesburg ilithibitisha kumiliki jengo hilo, ambalo imesema lilikuwa limetwaliwa na genge.

Chapisha Maoni

0 Maoni