Newcastle United yapangiwa vigogo michuano ya UEFA

 

Newcastle United imepangwa kuvaana na miamba ya Ulaya Paris St-Germain, Borussia Dortmund na AC Milan katika kundi F la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Newcaste iliyotinga katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu 2002-2003, inakutana na vigogo hao wa soka ambao wote wamewahi kufika fainali za michuano hiyo katika miaka 16 iliyopita.

Manchester United yenyewe imepangiwa kuivaa Bayern Munich, huku mabingwa watetezi wa michuano hiyo Manchester City wapo kwenye kundi moja na RB Leipzig.

Kwa upande wao timu ya Arsenal wamepangiwa kukutana na Sevilla huko nao Celtic wakikkutana na Atletico Madrid.

Chapisha Maoni

0 Maoni