Hatimae Rubiales ajiuzulu urais kwa kumbusu Hermoso

 

Rais wa Shirikisho la Soko la Hispania Luis Rubiales amejiuzulu wadhifa wake kufuatia kukosolewa kwa kumbusu mchezaji Jenni Hermoso wakati wa sherehe za ushindi wa Kombe la Dunia la Wanawake.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Hispania Hermoso, 33, amesema busu hilo alilopigwa baada ya Hispania kuifunga England, halikuwa la hiyari na ameshafungua mashtaka jumanne ya wiki iliyopita.

Katika taarifa yake Rubiales amesema amewasilisha barua yake ya kujiuzulu urais Shirikisho la Soko la Hispania kwa kaimu rais wa shirikisho hilo Pedro Rocha.

Chapisha Maoni

0 Maoni