Bosi hatari muuaji wa kundi la Mafia afariki kwa saratani

 

Bosi wa kundi la Mafia, Matteo Messina Denaro, ambaye alikuwa ni mhalifu anayetafutwa mno hadi alipotiwa nguvuni mwaka huu, afariki.

Denaro mwenye miaka 61, inaaminika kuwa ni bosi wa kundi hatari la Cosa Nostra Mafia alikuwa akivikimbia vyombo vya dola kwa miaka 30, hadi aliponaswa Januari mwaka huu.

Matteo Messina Denaro, alikuwa akitibiwa saratani wakati akiwa kizuizini na alihamishwa kutoka gerezani na kupelekwa hospitali mwezi huu.

Denaro anahusishwa na mauaji ya watu wengi, na aliwahi kunukuliwa akisema kwamba atayajaza makaburi miili ya maadui zake.

Chapisha Maoni

0 Maoni