Treni ya abiria yaacha njia na kuua watu 30 nchini Pakistan

 

Watu wapatao 30 wamekufa na wengine 100 kujeruhiwa baada ya treni kuacha njia yake kusini mwa Pakistan, msemaji wa jeshi la polisi amethibitisha.

Mabehewa kadhaa wa treni hiyo ya Hazara Express yamepinduka karibu na stesheni ya Sahara huko Nawabhsha, Kilomita 275 kutoka mji mkuu wa Karachi.

Abiria waliojeruhiwa wamepelekwa kwenye hospitali za jirani, ambapo waokoaji wanaendelea kujaribu kuwatoa watu waliokwama kwenye mabehewa yaliyoponeka.

Chapisha Maoni

0 Maoni