KOMBE LA DUNIA: Mabingwa watetezi Marekani watolewa na Sweden

 

Mabingwa watetezi wa kombe la dunia kwa wanawake timu ya Marekani imeduwazwa na Sweden kwa mikwaju ya penati huko Melbourne na kutolewa nje ya michuano hiyo.

Katika mchezo huo Marekani ilitawala dakika 120, lakini ilidhibitiwa na ubora wa kipa wa Sweden Zecira Musovic na mchezo kuishia bila kwa bila.

Katika mchezo huo Sweden walitupia wavuni penati tano na Marekani ikifunga penati nne, huku penati moja ya Sweden iliyofungwa kiutata ikiwabeba baada ya VAR kuikubali.

Chapisha Maoni

0 Maoni