Rais Dk. Samia anogesha zaidi Simba Day kwa Mkapa

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amenogesha Simba Day baada ya kutinga uwanjani akiwa mgeni rasmi na kupokelewa kwa shangwe na maelfu ya mashabiki wa timu hiyo.

Simba Day inaadhimishwa rasmi leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya wiki nzima ya shamra shamra na shughuli mbalimbali za kutoa kwa ajili ya jamii ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Maelfu ya mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es Salaam, wameendeleza rekodi ya kuujaza uwanja huo, ambapo kwa mujibu wa Simba tiketi zote zilimalizika siku tatu kabla ya leo.

Simba Sc katika kuadhimisha siku yao hiyo leo imewatambulisha rasmi kwa shamra shamra wachezaji wao wapya iliyowasajili kwa ajili ya msimu huu, na kukabiliana na Power Dynamos ya Zambia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwa amepozi katika picha ya pamoja na kikosi cha Simba SC.

Baadhi ya mashabiki wa Simba SC wakiwa na mabango yenye picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.

Chapisha Maoni

0 Maoni