Rais wa FIFA Infantino awananga walioikosoa FIFA

 

Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema mafanikio ya Kombe la Dunia la Wanawake yamewazima kidomodomo wakosoaji wa uamuzi wa kuongeza ushiriki wa mataifa 32 kwenye michuano hiyo.

Kulikuwa na wanaohoji kuongezeka timu kutoka 24, kuwa kungepelekea timu za upande mmoja kutawala katika michuano hiyo iliyofanyika Australia na New Zealand.

Hata hivyo, Nigeria, Afrika Kusini, Jamaica na Morocco, ambazo hazipo katika nafasi 40 ya ubora wa soka duniani, zilifanikiwa kuvuka hatua ya makundi.

Chapisha Maoni

0 Maoni