Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amekabidhiwa
msaada wenye thamani zaidi ya milioni 51 katika shule ya Msingi Mtakuja Wilaya
ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali
katika kuboresha sekta ya Elimu.
RC Chalamila amekabidhiwa madawati 200 kwa ajili ya Shule ya
Msingi Mtakuja, Miembeni, Kombo na vingunguti, Bati 400 shule ya msingi Airwing
na Sekondari karezange, Meza na viti vyake 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule
ya Sekondari Kivule na Gerezani pia meza na viti 34 kwa ajili ya walimu wa
shule ya msingi Bonyokwa,
RC Chalamila ameipongeza na kuishukuru Benki ya NMB kwa
msaada huo na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kusaidia maboresho katika
Sekta ya elimu katika Mkoa huo
Hata hivyo Mhe Albert Chalamila amepokea Changamoto zingine zilizowasilishwa
kwake na wanafunzi wa shule ya msingi Mtakuja ikiwemo ubovu wa miundombinu na
matundu ya vyoo ambapo ameutaka uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kutatua
Changamoto hiyo mara moja.
Aidha Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Dar es Salaam Bwana Dismas
Prosper akikabidhi msaada huo amesema msingi mzuri wa jamii unajengwa kupitia
upatikanaji wa elimu bora kama mdau mkubwa wa sekta ya elimu nchini tunaunga
mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika upatikanaji wa elimu bora
katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya Mhe Edward Mpogolo ameishukuru
Benki ya NMB kwa msaada huo ambao unalenga kuboresha sekta ya elimu katika
Wilaya ya Ilala, vilevile amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kutekeleza maelekezo na
maagizo yake kwa wakati.
0 Maoni