Wakazi wa mji wa Yellowknife wahaha kukimbia moto wa nyika

 


Wakazi wa mji wa Yellowknife kaskazini magharibi mwa Canada wameingia katika siku nyingine ya zoezi la kuhamishwa kuepuka maafa ya moto wa nyika uliopo umbali wa kilomita 15 kutoka mji huo.

Wakazi wapatao 20,000 wanatafuta namna ya kutoka kwenye mji huo, huku wengi wakiwa wao tayari wametumia magari yao kukimbilia miji mingine na baadhi wakitumia ndege za biashara.

Tayari wakazi wengine walisafirishwa kwa ndege za jeshi, katika kile kilichoolezwa kuwa ni oparesheni kubwa ya aina yake katika historia ya mamlaka za Kashazini Magharibi.

Chapisha Maoni

0 Maoni