Mwanamke jela miaka 22 kwa kumtumia barua ya sumu Trump

 

Mwanamke raia wa Canada amefungwa jela miaka 22 nchini Marekani kwa kosa la kutuma barua zenye sumu ya ricin, ikiwamo kwa Donald Trump wakati akiwa rais.

Mwanmake huyo Pascale Ferrier, 56, alikubaliana na hukumu hiyo Januari 2020, baada ya kukiri mahakamani makosa ya kutumia silaha za kibailojia.

Barua hiyo hatari iliyotumwa kwa Trump, iligundulika kabla ya kufika Ikulu ya Marekani (White House) Septemba 2020.

Mwana mama huyo Ferrier aliiambia Mahakama kwamba anajuta kuwa mpango wake huo ulishindwa na hakuweza kumdhuru Trump.

Chapisha Maoni

0 Maoni