Rais Dk. Samia awasili Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya Nanenane

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt, Samia Suluhu Hassan leo Agosti 07, 2023 amewasili Uwanja wa Ndege wa Songwe kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Siku ya wakulima (Nanenane) yatakayofanyika siku ya kesho Agosti 08 mkoani Mbeya.

Baada ya kuwasili Mhe. Samia amepokelewa na kusalimiana na viongozi mbalimbali waliojitokeza uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea.

Maonesho ya Siku ya Wakulima Nanenane kwa mwaka 2023 yameambatana na kauli mbiu isemayo “Vijana na wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula”.

Chapisha Maoni

0 Maoni