Tanzania na Malawi kujadili ushirikiano katika sekta ya nishati

 

Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga amesema Tanzania inatarajia kupokea ujumbe kutoka Serikali ya Malawi watakaofika nchini kwa ajili ya majadiliano kuhusu ushirikiano wa nchi hizo katika Sekta ya Nishati.

Mhandsi Luoga amesema hayo kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Felchesmi Mramba, wakati wa kikao cha maandalizi ya kupokea ujumbe huo kilichofanyika jijini Dar Es Salaam, Agosti 7, 2023 kwa kushirikisha maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake, Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Maji na Wizara ya Fedha.

Ujumbe huo utapokelewa na mwenyeji wao Waziri wa Nishati, January Makamba, unatarajiwa kuwasili nchini Agosti 9, 2023, utakaoshirikisha Waziri wa Nishati wa nchi hiyo na Viongozi wengine waandamizi katika masuala ya Nishati na Maji kutoka nchini humo. 

Chapisha Maoni

0 Maoni