Nigeria watolewa nje kombe la dunia wanawake na England

 

England imefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake kwa mikwaju ya penati na kuwatoa nje ya michuano hiyo timu ya Nigeria.

Katika mchezo huo ulioisha kwa timu zote kutofumania nyavu katika dakika 120, England iliibuka washindi kwa mikwaju ya penati 4-2.

Georgia Stanway alitoa nje mkwaju wa kwanza kwa England, lakini Nigeria nayo ikapoteza mikwaju miwili ya penati iliyofuata, na Chole Kelly alipiga mkwaju wa mwisho ulioipa ushindi England.

Katika kuchanganyikiwa James alimkanyaka Michelle Alozie mnamo dakika ya 87 baada ya kupokonywa mpira na refa kumpatia kadi nyekundu baada ya kuangalia VAR.

Chapisha Maoni

0 Maoni