PLASCO kuipatia Muhimbili tanki kubwa la lita 200000

 

Timu ya wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetembelea kampuni ya PLASCO Tanzania, ambayo ipo mbioni kutoa msaada wa tanki la maji lenye ujazo wa lita laki mbili.

Tanki hilo linathamani ya shilingi milioni 150, litasaidia katika kutatua changomoto ya ukosefu wa maji ambayo huwa inaikabili hospitali hiyo ya taifa hasa wakati wa kipindi cha kiangazi.

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa MNH Mhandisi Jonas Bayona amesema lengo la ziara hiyo ni kujionea teknolojia mpya ya utengenezaji matanki, kujifunza namna ya kutumia na kurekebisha pale inapotokea changamo yoyote.

Chapisha Maoni

0 Maoni