Ni kweli wanaume wenye midevu wanamvuto?

 

Je, ndevu kwa wanaume zinaongeza mvuto? Katika miaka ya hivi karibuni ndevu zimekuwa ni fasheni ya muonekano kwa wanaume Watanzania, ambapo wasioweza kuzikuza kwa asili, hulazimika kuzikuza kwa kutumia dawa ama kupandikiza kwa gharama.

Soko la urembo wa kuboresha muonekano wa sura za wanaume nchini nalo haliko nyuma limelazimika kuchangamkia fursa hii na wajasiriamali wamekuwa wakitengeneza fedha kwa kuuza mafuta ya kukuziwa ndevu.

Kama ilivyo kwa wanawake kupaka vipodozi katika kuboresha muaonekano wa sura zao ili kuongeza mvuto (sexiness) na kujiamini, wanaume nao pia wameanza kufanya hivyo kwa kuboresha wingi wa ndevu zao.

Chapisha Maoni

0 Maoni