NHIF yapima na kutoa elimu ya afya bure Nane Nane Mbeya

 

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), unawahimiza wananchi wa mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani kufika katika banda lake kwenye maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale ili kupata huduma za upimaji na elimu ya afya bure.

Rai hiyo imetolewa na Meneja Uhusiano wa NHIF Bi. Anjela Mziray ambaye ameeleza kuwa, suala la kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ni la msingi kwa kila mtu na Mfuko unachangia juhudi za Serikali kwa kutoa huduma za upimaji bure na kutoa elimu ya kuepukana na magonjwa hayo katika ushiriki wake kwenye maonesho ya Nanenane.

"Tupo hapa kwenye viwanja vya John Mwakangale ndani ya Mabanda ya Taasisi za Umma, tunawahimiza wananchi na washiriki wa maonesho haya kufika hapa na kupima na kujua hali za Afya zao na kupata elimu mtindo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza," alisema Anjela.

Vipimo vinavyofanyika bandani hapo ni pamoja na Shinikizo la damu, sukari na hali lishe na kisha wananchi kupatiwa matokeo ya vipimo.

Chapisha Maoni

0 Maoni