Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC Ayoub Chamshama afariki dunia

 

Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC Ayoub Chamshama amefariki dunia nchini India alipokuwa amepelekwa kupatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo hicho imetolewa na mtoto wake Soud Ayubu Chamshama wa Chang'ombe Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imesema kifo cha Chamshana kimetokea tarehe 11 Agosti 2023 nchini India alipokuwa kwa matibabu.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 15 Agosti 2023 kijijini kwao Kilole, Lushoto, Mkoani TANGA.

Enzi za uhai wake marehemu Chamshama alishika nyadhifa mbalimbali. Alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni ya Tanzania Tea Blenders, vilevile alihudumu kwa muda mrefu kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC na pia alikuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke.

Chapisha Maoni

0 Maoni