Mwanaume mzungu awauwa kwa risasi watu watatu weusi

 

Mwanaume mwenye silaha, amewauwa watu watatu weusi katika shambulizi la kibaguzi na kisha yeye mwenyewe kujiua huko Jacksonville, Florida, mkuu wa polisi amesema.

Mwanaume huyo mzungu mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka 20, aliingia kwenye stoo ya Dollar General The man, na kuwafyatulia risasi watu wenye asili ya weusi.

Mkuu wa Polisi T K Waters ameeleza kuwa wanaume wawili na mwanamke mmoja wameuawa na mzungu huyo kijana, ambaye alikuwa amevaa vazi la kuzuia risasi na ujumbe wa kibaguzi.

Meya wa Florida Donna Deegan, amesema kwamba ni tukio la uhalifu wa chuki, lililochangiwa na msukumo wa chuki za kibaguzi.

Chapisha Maoni

0 Maoni