Moshi mweupe wamfukiza Askofu Malasusa KKKT

 


Moshi mweupe umemfukiza Askofu Alex Malasusa katika Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilitheri Tanzania (KKKT)  na kuchaguliwa kuwa Askofu mkuu wa kanisa hilo.


Askofu Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani anachukua nafasi ya Askofu Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozo wa awamu mbili aliyemaliza muda wake.


Askofu Malasusa (62) amerudi tena kushika wadhifa huo ambao aliutumikia kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka 2007 hadi 2016.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi huo,Askofu Amon Mwenda,amesema kura zilizopigwa zilikuwa 241 ambapo kati ya hizo Askofu Malasusa amepata kura 167 sawa na asilimia 69.3 huku Askofu Abednego Kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3.

Chapisha Maoni

0 Maoni