Mgombea urais nchini Ecuador katika uchaguzi ujao aliyekuwa akipiga
kampeni ya kupiga vita rushwa na magenge ya uhalifu, amepigwa risasi na kufa
akiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea huyo Fernando Villavicencio, ambaye ni mbunge wa
bunge la nchi hiyo, alishambuliwa kwa risasi wakati akiondoka kwenye mkutano wa
hadhara Jijini Quito, Jumatano.
Mgombea huyo ni mmoja kati ya waliotoa madai ya kuwapo kwa
uhusiano baina ya makundi yanayoratibu uhalifu na maafisa wa serikali ya
Ecuador.
Genge la uhalifu la Los Bobos ama Mbweha lenye wafuasi 8,000
nchini humo, ambao wengi wao wanatumikia vifungo magerezani limedai kuhusika na
shambulizi hilo.
CHANZO: BBC
0 Maoni