Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii ni kama limekamilika

 


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amefanya ukaguzi wa mwisho mwisho wa jengo jipya la ghorofa 5 la Wizara ya Maliasili na Utalii Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

Jengo hilo limekamilika na kwa sasa zinafanyika hatua za mwisho za kufanya majaribio mbalimbali ikiwemo vifaa vya umeme, ulinzi na mawasiliano kabla ya wafanyakazi kuhamia rasmi hivi karibuni.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi akipewa maelezo wakati akikagua kwa nje jengo jipya la ghorofa 5 la Wizara ya Maliasili na Utalii Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

Chapisha Maoni

0 Maoni