Beki wa Simba Inonga kufanyiwa vipimo zaidi leo

Beki wa kati wa Simba Hennock Inonga leo atafanyiwa vipimo kubaini ukubwa wa jeraha alilopata jana wakati timu ya Simba ikiibua na ushindi wa mkwaju ya penati 4-2 dhidi ya Singida Faountain Gate.

Hennock alishindwa kumaliza mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fauntain Gate jana baada ya kuumia bega.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Inonga atafanyiwa uchunguzi wa kitabibu leo, Wanasimba watapewa taarifa kuhusu hali yake

"Ni kweli Inonga aliumia jana, alitoka uwanjani akiwa na maumivu makali sana ya bega. Alipatiwa huduma ya kwanza, sasa anaendelea vizuri. Kesho (leo) madaktari watamfanyia uchunguzi kubaini ukubwa wa jeraha ili kuona kama atahitaji matibabu zaidi au la," alisema Ally.

Simba ilitinga fainali ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mkikwaju ya penati 4-2 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Singida Fauntain Gate.

Siku ya Jumapili Simba itachuana na Yanga katika mchezo huo wa finali ya Ngao ya Jamii, katika dimba la Mkwakwani Tanga

Chapisha Maoni

0 Maoni