Kapteni wa Uingereza Harry Kane anajiandaa kufanyiwa vipimo
vya afya na klabu ya Bayern Munich baada ya kupewa ruhusa na klabu yake ya
Tottenham kwenda Ujerumani.
Timu za Bayern na Spurs zimekubaliana mauzo ya paundi
milioni 86.4 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hapo jana.
Uamuzi wa kuhamia Bayern umebakia sasa kwa Kane, ambaye ni mfungaji
bora aliyeifungia Spurs magoli 280 kwenye michezo 435.
Kane ana mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake na kunauwezekano
asiweze tena kubakia kwenye klabu hiyo.

0 Maoni