Nchi ya Sweden imeonyesha kiwango bora na kufanikiwa kutinga
nusu fainali ya kombe la dunia wanawake kwa kuifunga Japan magoli 2-1.
Japan ilikuwa inaonekana kama inania ya kutwaa kombe hilo,
baada ya kutinga hatua ya 16 bora kwa kuifunga timu ya Norway.
Katika mchezo wa leo Japan walifungwa goli la kwanza na Amanda
Ilestedt na kisha kiungo wa Manchester City Filippa Angeldahl kuongeza goli la
pili kwa mkwaju wa penati
Japan walipatiwa penati yenye utata lakini mkwaju uliopigwa
na Riko Ueki dakika ya 76 uligonga mwamba, ndipo baadae Honoka Hayashi akaifungia
Japan goli pekee dakika ya 87.
0 Maoni