Jaji Kazi ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amemteua Jaji George Joseph Kazi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar, Jaji Kazi ataapishwa tarehe 28 Agosti, 2023 saa 8 Mchana Ikulu Zanzibar pamoja na wajumbe wa Tume hiyo. Uteuzi wake unaanza leo 24 Agosti, 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni