Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (1) cha Kanuni ya Adhabu (Penal
Code), mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au
popote, atakuwa ametenda kosa la uhaini iwapo ataamua:
* Kujaribu kumuua Rais
* Kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) cha Kanuni ya Adhabu (Penal
Code), mtu yeyote akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, ambaye anajenga
nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea,
anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au
kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo yafuatayo, atakuwa
ametenda kosa la uhaini:
* Kusababisha kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au
kumzuia Rais
* Kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika
wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi,
Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya
Muungano
* Kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano; au
* Kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na
Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kubainisha nia hiyo kwa
kuchapisha maandishi au machapisho au kwa kitendo chochote cha siri
kinachojionyesha cha hali yoyote
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (3) cha Kanuni ya Adhabu (Penal
Code), mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano, atakuwa
ametenda kosa la uhaini kwa:
* Kuwa na mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au
kwingineko
* Anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au
kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au
* Anabeba silaha
ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia,
kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi
wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (4) cha Kanuni ya Adhabu (Penal
Code), mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani
ya Jamhuri ya Muungano au popote, atakuwa ametenda kosa la uhaini kwa kuonesha
nia ya kumsaidia adui wa Jamhuri ya Muungano kwa kufanya kitendo chochote
kinacholenga au kinachoweza kutoa msaada kwa adui huyo, au kuingilia kwa
maelekezo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, au kuzuia operesheni ya Majeshi
ya Ulinzi au Jeshi la Polisi, au kuhatarisha maisha, ana hatia ya kosa la
uhaini.
⚠️ Adhabu ya kosa la uhaini ni
kifo
✒️ Kanuni hii ya adhabu ni kwa
mujibu wa Sheria ya Uhaini Namba 2 ya mwaka 1970
0 Maoni